Hivi Ndivyo Unavyozidi Kuteketeza Maisha Yako Bila Ya Kujua.
Ukiwasha mshumaa utawaka huku ukitoa mwanga na joto. Lakini kadri muda unavyoendelea mshumaa huo utazidi kuwaka huku ukiendelea kupungua na kama hautazimwa, utaisha kabisa. Ukishaisha hutaweza kuurejessha tena na kuutumia. Kitendo hiki cha kutumia mara moja bila ya kuwa na uwezo wa kurejesha huitwa kuteketea.
Maisha yako ni kama mshumaa unaowaka. Mshumaa wa maisha yako una muda maalumu wa kuwaka. Kadri unavyopewa uhai kila unapoamka ndivyo muda wa mshumaa wako kuwaka unvyozidi kupungua na ipo siku mshumaa huo utazima kabisa. Mtu aliyewasha mshumaa hatasikitika kama utatimiza lengo lake. Kama atauwasha mshumaa huo na kuweka gizani utaangaza gizani na kutimiza lengo la kuleta nuru. Lakini itakuwa ni hasara kama mshumaa huo utawashwa na kuendelea kuwaka juani kwa lengo la kuleta mwanga.

Wewe kama mshumaa je unaendelea kuwaka kwa faida au kwa hasara? Je unawaka gizani au unawake juani na kuleta hasara? Thamani ya maisha yako ipo kwenye muda, kadri unavyosema unaishi ndivyo unavyozidi kutekeza maisha yako. Kumbe thamani ya maisha yako ipo kwenye muda. Utayateketeza maissha yako kwa faida kama utautumia muda wako vizuri kwa kuwang’azia watu wengine yaani kuwapa thamani watu wengine, huko ndiyo kutakuwa kuteketeza maisha yako kwa faida.
Namna pekee ya kutumia muda wako vyema kisha kuyateketeza kwa faida ni kuishi kusudi la maisha yako. Kila kiumbe kilichopo duniani kina sababu maalumu ya kuwepo. Tazama hata wadudu kama nyuki, bila nyuki tusingekuwa na asali ambayo ni miongoni mwa vitu vitamu sana. Ardhini kuna wadudu wengi wanaohakikisha wanaozesha vitu na kuwa katika hali ambayo unaweza kuivumilia. Fikiria kama kusingekuwa na viumbe hivyo, dunia nzima ingekuwa inanuka kwa mizoga. Kama viumbe hao wadogo wana kazi maalumu na thamani kubwa, wewe je si zaidi ya hao?
Mungu aliona uhitaji duniani, ndiyo maana akakuumba na kukuleta hapa duniani ili uweze kutoa thamani ya kutimiza uhitaji huo. Hivyo hupo hapa kwa bahati mbaya. Hiki ndicho unachotarajiwa ukikamilishe. Utafanikiwa kuishi maissha yako kiukamilifu kama utatambua kazi hiyo maalumu uliyonayo kisha kuifanya. Usiishi kwa kufanya tu kilichopo mbele yako, huku ni kuamua kuteketea bila kujua na bila faida.
Katika kuliisshi kusudi lako umepewa muda maalumu wa kulitimiza. Muda huo unateketea kila kukicha, na hautaacha kuendelea kuteketea. Kitu pekee cha kufaidi ni kuutumia vizuri muda huo kwa kutoa thamani kwa watu wengine iliyobebwa na kusudi lako. Je muda wako umeteketea kwa kiasi gani mpaka sasa? Je na wewe umewasha mshumaa kisha kuweka juani uangaze nuruni? Je umekuwa bussy kuiga wanachokifanya watu wengene huku muda wako ukiendelea kuteketea ungali hujaanza jukumu lako maalumu?
Wakati umefika sasa wa kuteketeza maisha yako kwa faida. Umeyachezea maisha yako vya kutosha. Fanya bidii kutambua kusudi lako na anza kuliisshi mara moja kabla mshumaa wako haujazima. Je kuna jambao gani unatamani ulikamilisshe kabla hujafa? Je kuna hali gani ambayo ukiiona moyo wako hautulii ukiitamani uibadilishe bila kujali ukubwa na ugumu unaoweza kukutana nao? Huko ndiko kusudi lako lilipo. Ukikamilisha hilo utakuwa umeteketeza maisha yako kwa faida kwa kuwapa thamani watu wengine.
Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI kimeelezea kiundani jinsi ya kutambua kusudi lako na kuliisshi kikamilifu. Bei ya kitabu hiki ni shilingi elfu kumi(sh 10,000/-) tu. Pata naka la yako leo kwa kupiga simu namba 0752206899.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz
