Mruhusu Huyu Aishi Maisha Yako.Mruhusu Huyu Aishi Maisha Yako.
“Hata kama mtasimama watu wengi, bado kila mtu atatengeneza kivuli chake”Ukisimama sehemu yenye mwanga upande mmoja nyakati za usiku kivuli kitatokea. Mtu mwingine akisogea mahali hapo, kivuli kingine kitajitokeza. Hata pale watu kumi watakaposogea bado kila mtu atatengeneza kivuli chake. Hii inamaanisha kuwa hakuna namna yoyote mtu anaweza kuzalisha kivuli [...]
