Kwani Wewe Umejaribu Mara Ngapi?


Categories :

Kila kitu ninachokifanya hakitiki! Kwani umejaribu mara ngapi?

Mimi nyota yangu imefifia inabidi niende kwa mtaalamu aisafishe, mambo yangu hayaendi! Kwa umejaribu mara ngapi?

Nilitaka kuwa mbobezi kwenye eneo hili lakini naona kama nipo palepale. Kwa wewe umefanya kwa muda gani?

Nimefanya muda mrefu sana lakini sipati majibu, sasa naacha. Kwani umefanya kwa muda gani?

Moja ya sababu kubwa ya watu kutopata kitu wanachokita na mtazamo ule wa kupata kwa haraka na kwa urahisi.

Mtu hutaka aanze biashara leo na ndani ya mwezi mmoja tu iwe inafahamika na kukua sana. Jambo hilo ni gumu sana.

Mtu hutaka kuanza kujifunza leo na ndani ya muda mfupi tu awe mbobezi. Jambo ambalo haliwezekani.

Mtu hutaka kuanza kuweka juhudi leo na baada ya muda mfupi tu awe na mafanikio makubwa. Mafanikio makubwa hayaji kwa haraka hivyo.

Mgunduzi wa taa za umeme, Thomas Edison ambazo mwanga wake tunaufurahia leo alifanya katribani majaribio elfu kumi kabla ya kugundua taa hiyo. Alifanya hivyo bila kukata tamaa. Wewe umejaribu mara ngapi mpaka umeamua au unataka kukata tamaa?

Thomas alipoulizwa kuhusu kushindwa kwake alisema “ I have not failed. I have just found 10,000 ways that won’t work.” ikiwa na tafsiri kuwa sijashindwa. Nimejua njia 10,000 ambazo hazitafanya kazi kabla ya kukutana na inayofanya kazi.

Kushindwa kwako ndiyo njia ya kuelekea kule kwenye mafanikio.

Jambo la pekee la kukufikisha huko ni kutokukata tamaa. Chukulia kukata tamaa ni dhambi kubwa mbele zako.

Kila unapofanya kitu na kushindwa jifunze kitu na rudi ukiwa bora zaidi ya mwanzo.

Kama unataka ubobezi, jipe muda. Huchukua miaka kumi au zaidi kupata matokeo makubwa au kuwa mbobezi kwenye kile unachofanya.

Chagua kitu kimoja leo ambacho utajitoa mzima mzima na kukifanya kwa muda mrefu bila kukata tamaa.

Je ni kujenga utajiri?
Je ni kujenga ubobezi?
Je ni kujenga biashara kubwa?
Je ni kujenga taasisi kubwa?

Muhimu chagua kile unachokipenda na weka maisha yako yote mpaka kikulipe. Unachagua nini leo?
ANZA LEO ANZA SASA ANZA NA ULICHONACHO.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *