Ukimkaribisha Huyu….Umepata Vyote Maishani Mwako


Categories :



Mama mmoja alitoka nje muda wa mchana na kukuta wanaume watatu nje wenye ndevu ndefu. Alivyowaona, akahisi kuwa lazima wangekuwa na njaa kwa muda huo.

Akaamua awakaribishe ndani ili aweze kuwapa chakula wale. Ndipo wakamuuliza kama mme wake alikuwa ndani. Mke akajibu kuwa mme wake hayupo, ameenda kazini. Wakamuambie kuwa wasingeweza kuingia mpaka mme wake awepo.

Mme wake aliporudi nyumbani, yule mama alimweleza kile kilichotokea. Ndipo mme wake alipomwambia kuwa sasa aende akawaambie amerudi hivyo waingie ndani ili wapate chakula.

Mama alitoka na kuwaeleza kuwa sasa mme wake amesharudi hivyo waingie ndani. Kabla ya kuingia, mmoja alijitambulisha kuwa yeye anaitwa Bw. Utajiri, na kuwatambulisha wenzake kuwa mmoja anaitwa Mafaniko na mwingine anaitwa Upendo.

Aliendelea kumueleza yule mama kuwa wanapaswa kuchagua mmoja atakayeingia ndani kwani hawawezi kuingia wote. Mama alishangaa sana, ndipo aliingia ndani ili kujadiliana na mme wake.

Baada ya kumueleza mme wake, mme wake akasema tuchague utajiri ili nyumba yetu ijae utajiri. Mke wake akasema hapana , ni afadhali tuchague mafanikio ili nyumba yetu ijazwe na mafanikio. Machaguo haya yalimuibua bintiyo alikokuwa. Akasema hapana tumchague Upendo aingie ili nyimba yetu ijazwa na upendo.

Ndipo mama yule alipotoka na kumwaambia wale wanaume watatu kuwa wamechagua upendo. Baada ya upendo kuanza kuingia, akashangazwa kuona na wale wawili wanamfuata upendo. Ndipo alipowauliza hii ni nini? Wakamjibu kuwa wangechagua itajiri au mafanikio, angeenda huyo huyo. Lakini kwa sababu wamechagua upendo, hawezi kwenda pekeyake kwani kila palipo na upendo lazima na sisi utajiri na mafanikio tuwepo.

UPENDO ni chanzo cha kila kitu maishani. Ukiwa na upendo wa dhati umepata kila kitu.

1. Mpende muumba wako naye atakuambia upekee wa kupatia mafanikio ya kipekee

2. Jipende mwenyewe ndipo utajijua wewe halisi

3. Mpende jirani kwanzo ndipo utampa thamani ya kubwa sana lakini yeye atakupa utajiri.

4. Kipende kwa dhati unachokifanya ndipo utakifanya kwa ubora mkubwa sana kisha kupata matokeo makubwa sana.

5. Karibusha upendo kwenye biashara yako. Wateja watang’ang’ania kubaki kwenye biashara yako na kukupa mauzo ya kudumu.

Karibisha upendo kwenye familia yako. Maelewano huleta utulivu wa fikra. Utulivu wa fikra huleta mafanikio.

Ndugu! Kuanzia sasa tanguliza upendo kwenye kila unachofanya. Utakifanya kwa ubora wa hali ya juu. Ukifanya kwa ubora wa juu, utajiri na mafanikio vitakuja kwenye maisha yako.

Karibu sana.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *