Hii Ndiyo Njia Pekee Ya Kuishinda Hofu Iliyosimama Kabla Ya Mafanikio Yako….
Kama kuna kitu kimoja kimekukwamisha kufika ulikotakiwa kuwa sasa basi ni hofu.
Kama kuna hofu kubwa ambayo imekuwa kikwazo kwako kufikia mafanikio makubwa unayostahili basu ni hofu ya kushindwa.
[ ] Hujaweka malengo makubwa mwaka huu ukihofia utashindwa.
[ ] Hujaanzisha biashara ukihofia utapata hasara.
[ ] Hujawafikia watu waliokuzidi mafanikio ukihofia utashindwa kuwashawishi.
[ ] Unaendelea kufanya uliyoyazoea kwa sababu unahofia ukifanya kwa utofauti unaweza kushindwa.
[ ] Hujaanza kufanya uwekezaji ukihofia unaweza usifanye vizuri kisha ukapata hasara.
Kuna matokeo yako halisi unayostahili yapo mbele ya vitu unavyovihofia.
Kumbuka kuwa vitu vingi unavyovihofia huwa havitokei na hata kama vikitokea si kwa ukubwa wa uliovipa.
Kuna njia moja ya pekee ya kukabiliana na kuiishinda hofu kisha kuanza kuishi maisha unayostahili.
Njia hiyo ni; kufanya kile unachokiogopa. Ni hivyo tu na hakuna njia ya mkato.
Kama kuna kitu umekuwa ukikihofia kwa muda mrefu na hujakifanya mpaka, leo basi ni kwa sababu hujajipa ujasiri wa kuanza kukifanya.
Unachotakiwa kukifanya ni kuiambia akili yako kuwa hakuna njia nyingine ya kupata matokeo zaidi ya kuanza kukifanya. Pia iambie akili yako kuwa unachokihofia hakipo.
[ ] Mwaka ndiyo unazidi kwenda….anzisha biashara uliyopanga kuianzisha 2024.
[ ] Anza kuwekeza hata 10% ya kipato chako kwenye hisa, vipande, akaunti maalumu…..
[ ] Nenda kamuone mtu muhimu uliyemhofia siku nyingi.. ..
[ ] Nenda kaanzishe jambo jipya uliloliogopa kwa siku nyingi, litakupa matokeo mapya kabisa
Kadri unavyozidi kuahirisha kuchukua hatua unayoihofia ndivyo unavyozidi kuikuza hofu hiyo;
Chukua hatua Leo Chukua hatua Sasa, anza hata kwa udogo.
Kusoma makala zaidi ya 500 kuhusu UWEZO na MAFANIKIO bonyeza hapa www.amshauwezo.co.tz ni bure kabisa.
” Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz
