Author: amshauwezo

Unayaumiza Macho Yako Bure! Tumia Akili Kuona Gizani.Unayaumiza Macho Yako Bure! Tumia Akili Kuona Gizani.

Mtu ambaye ameshapita barabara fulani mara nyingi bila kupotea, ana uwezo wa kurudi nyumbani hata usiku wa manane kukiwa na giza nene bila ya kupotea. Dereva ambaye ameshaendesha gari kwenye barabara fulani, si rahisi kupata ajari au kuingiza gari kwenye makorongo ya barabara hiyo kwani anakuwa anaifahamu barabara hiyo vizuri [...]

Huwezi Kung’aa Kwa Kupaka Mafuta Taswira Yako Unayoina Mbele Ya Kioo.Huwezi Kung’aa Kwa Kupaka Mafuta Taswira Yako Unayoina Mbele Ya Kioo.

Ukisimama mbele ya kioo cha kujitazamia utajioni jinsi ulivyo. Hata chochote utakacho kuwa unafanya wewe, taswira yako pia itakuwa inakifanya. Ukitabasamu na taswira yako itatabasamu, ukinuna kadhalika taswira yako itanuna. Kwa hiyo chochote utakachokuwa unafanya wewe na taswira yako itaitikia. Lakini kitu cha ajabu ni kuwa ni taswira itakayokuwa inakuitikia [...]

Ngazi Tayari Unayo, Kwa Nini Hupandi Juu?Ngazi Tayari Unayo, Kwa Nini Hupandi Juu?

Kama upo sehemu na unataka kupanda sehemu ya juu zaidi, unaweza kutumia kifaa kama ngazi kupanda huko. Urefu wa ngazi ndiyo unaweza kuamua wapi ufike. Kama ukimuona mtu yupo chini na analalamika kuwa anashindwa kupanda juu wakati ngazi ipo pembeni yake, ungemshangaa sana. Yamkini na wewe ungemlaumu sana na kumuambia [...]

Ulichonacho Sasa Ndicho Kinachokuzuia Kupata Unachostahili.Ulichonacho Sasa Ndicho Kinachokuzuia Kupata Unachostahili.

Kuna mafanikio fulani ambayo umeshayapata mpaka sasa. Unastahili kujipongeza au kupongezwa kwa ajili ya hayo. Lakini ukilinganisha kile ulichokipata na kile ulichostahili, kuna safari ndefu unayotakiwa kupiga. Kuna mazingira ambayo mafanikio ya sasa au vitu vingine ulivyonavyo vimekuwa vikwazo kupata ulichostahili. Umekuwa ukitafuta aliyesababisha kutoyafikia mafanikio yako makubwa uliyostahili, lakini [...]

Hii Ndiyo Sababu Ya Kwa Nini Kila Pampu Yako Haitoi Mafanikio.Hii Ndiyo Sababu Ya Kwa Nini Kila Pampu Yako Haitoi Mafanikio.

Kuna kijiji kimoja kilichokuwa na ukame mwingi na hivyo kufanya kuwana shida ya maji. Watu walilazimika kutembea umbali mrefu ili kupata maji. Baada ya kilio hicho cha siku nyingi ufadhili ulipatika ambapo kuna shirika moja lilijitokeza na kutoa msaada wa kuchimba visima na kuweka pampu za mkono za kuvutia maji [...]

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kukaa Kwenye Moto Wa Tanuru Na Kupata Kile Unachokitafuta.Hivi Ndivyo Unavyoweza Kukaa Kwenye Moto Wa Tanuru Na Kupata Kile Unachokitafuta.

Tofari bichi halina thamani likiachwa hivo hivyo bila kupitishwa kwenye tanuru. Ila likiwekwa kwenye tanuru kisha likavumilia moto mkali uliopo huungua na kuiva kisha kuwa na thamani kubwa. Thamani ya tofari hilo huongezeka na kuwa kubwa kulingana na ukubwa wa moto. Ndiyo maana zile tofari zitakazokaa karibu na moto na [...]