Huwezi Kuonyesha Ufundi Wako Wa Kuogelea Kwa Kuogelea Mavumbini Rudi Majini.Huwezi Kuonyesha Ufundi Wako Wa Kuogelea Kwa Kuogelea Mavumbini Rudi Majini.

Ukiongelea ufundi wa kuogelea majini huwezi kuacha kumtaja samaki. Hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutembea majini na kuepuka vikwazo vyote vilivyomo. Licha ya uwezo huo mkubwa alionao samaki lakini hawezi kuuonyesha mavumbini.  Ukimchukua samaki na kumweka nchi kazu unaweza kusema sio yeye yule anayeogelea kwa ufundi mkubwa [...]

Kuna mahali pa kuanzia, mahali penyewe ni hapo ulipo.Kuna mahali pa kuanzia, mahali penyewe ni hapo ulipo.

Licha ya watu kuwa na ndoto kubwa ya kuishi maisha fulani, lakini wam Wamekuwa ekuwa wakiainisha sababu za kwa nini hawawezi kuishi ndoto hizo. na sababu ambazo zinatengenezwa na kuona ni za ukweli kabisa. Sababu mojawapo imekuwa kutokujua wapi kwa kuanzia. Imekuwa rahisi kukutana na mtu akakuambia hajui aanzie wapi [...]

Fikra Zako Zisizoonekana Kwa Macho Ndizo Zilizojenga Maisha Yako Yanayoonekana Kwa MachoFikra Zako Zisizoonekana Kwa Macho Ndizo Zilizojenga Maisha Yako Yanayoonekana Kwa Macho

Kuna vitu tunavyoviona kwa macho na kuishia kuvishangaa, kuvipenda au kuvichukia. Vitu hivyo ni pamoja n vile ulivyovizalisha mwenyewe. Licha ya kuhusika kuvizalisha lakini wewe mwenyewe umekuwa mstari wa mbele kuvishangaa, kuvichukia na mara nyingine kuvidharau. Umeenda mbali zaidi kwa kuwalalamikia watu wengine  bila kujua wewe ndiye uliyevizalisha. Vitu vyote [...]

Je Umekuwa Ukisubiri Muda Au Ukipoteza Muda?Je Umekuwa Ukisubiri Muda Au Ukipoteza Muda?

Kusubiri au kupoteza muda ni jambo ambalo limekuwa linafanywa na watu kwa kujua au kutokujua. Mara nyingine mtu amefikiria anasubiri wakati kumbe  kiuhalisia anapoteza muda. Kusubiri muda ni pale unapongoja kupata mrejesho baada ya kuweka nguvu kwenye jambo fulani. Hii ni sawa na kutanguliza thamani  huku ukitarajia majibu ya thamani [...]

Siku Ambayo Kobe Atamsusia Jirani Yake Nyumba Yake Ndiyo Utakuwa Mwisho Wa Uhai WakeSiku Ambayo Kobe Atamsusia Jirani Yake Nyumba Yake Ndiyo Utakuwa Mwisho Wa Uhai Wake

Kobe ni mnyama ambaye mgongo wake umefunikwa na magamba magumu ambayo siyo rahisi kuyavunja. Mgongo huo huonekana kama nyumba kwake kwani akihisi hatari yoyote ile hujikunja ndani huku akizamisha kichwa na miguu yake na gamba tu ndilo linabaki likionekana. Hivyo mgongo huo ni nyumba inayotembea kwani huwepo popote alipo. Kwa [...]