Usiendelee Kuishi Na Yeye Feki, Baki Kuwa Wewe Halisi
Licha ya kwenda mbele ya kioo na kujitazama lakini bado ukitazama ndani yako unaweza kumuona mtu mwingine tofauti na yule uliyemuona mbele ya kioo cha kujitazamia.
Ø Je umekuwa ukiishi lakini unaona kama kuna mtu mwingine zaidi ya ulivyo sasa?
Ø Je upo sehemu lakini huwa unajiona kuwa kuna sehemu nyingine ambayo ulitakiwa kuwepo?
Ø Je kuna kazi unafanya lakini kila wakati unahisi kuna kazi nyingine ambayo ulitakiwa uwe unafanya
Ø Je kuna mengi umeyakamilisha hapa duniani lakini bado unajiona una deni?
Ø Je una mali nyingi lakini bado unahisi ni mtupu?
Inawezekana kuna hali nyingi zaidi ya hizi unazipitia katika maisha yako kiasi cha kuona kama ndani yako kuna watu wawili na anayejionyesha sana kwako siyo yule unayeridhika naye. Kama upo kwenye hali hiyo tambua kuwe yeye ndiye anayeishi maisha yako na sio wewe halisi.
Ndugu uliumbwa ukiwa kwa lengo la kuwa wewe halisi, mwenye upekee yaani ukiwa hufanani na mtu yoyote, mwenye nguvu za kipekee ndani yako kiasi kwamba kama nguvu hizo zingetumika ungekuwa umeshafanya mambo makubwa ambayo wewe mwenyewe ungeshaa pamoja na dunia.
Lakini bahati mbaya amejitokeza mtu mwingine ambaye leo ngoja nimwite ‘yeye’ Huyu muda mwingi amekuziba wewe halisi usionekane. Huyu ni feki na sio orijino kama wewe halisi. Hivyo namwita yeye feki; ndiyo maana wewe halisi ukitazama mambo mengi huridhiki nayo na unabaki unashanga .
Ø Yeye feki amekuziba wewe halisi kwa kukulazimisha uwe unaiga maisha ya watu wengine na hivyo umehindwa kuonyesha upekee wako!
Ø Yeye feki ameziba ndoto zako, umekosa maono ndiyo maana unaishi maisha ya leo tu. Kila siku unaishi maisha yoyote yanayokuja mbele yako!
Ø Yeye feki amekufanya kuwa mtu wa kawaida, huna maajabu yoyote, ndiyo maana mara nyingine unahangaika kujulikana hata njia zisizo halali!
Ø Yeye feki amekuziba usitumie kipaji chako, umeiga wanavyofanya wengine kisha umeamabulia kutoa thamani ndogo na hivyo kuwa na maisha ya kawaida. Hii imekufanya kukosa uhuru wa kifedha sasa na wala huna matarajio.
Ø Yeye feki amekufanya uwe bise kuwafuatilia na kuwasikiliza wengine. Hizi ni kelele zilizosababisha kuto jisikiliza wewe halisi. Hivyo wewe sio halisia umekuwa yle feki.
Ndugu kuna mabadiliko makubwa sana yatatokea maishani mwako pale utakapoamua kumfukuza yeye feki na kubaki wewe halisi. Hata kama yeye feki ameishi ndani yako kwa muda mrefu, bado una nafasi ya kugeuka kuwa wewe na kufaidi uorijino wako
Sawli la kwanza unalotakiwa kujiuliza ni kuwe wewe wa sasa ni orijino au feki? Utajua kama kuna thamani kubwa ambayo umeibeba kwa ajili ya dunia, kama unaridhika na hicho unachokifanya, kama unaona kuna thamani kubwa unaitoa sasa au utaanza kuitoa na kukupa uhuru wa fedha. Je kuna upekee unauonyesha katika maisha yako.
Kaa chini leo, sehemu ya utulivu kisha jiulize nani amenitawala?mimi ni orijino au yeye feki? Kisha sikiliza moyo wako. Unapenda kufanya nini? Kitu gani unatamani ukipate maishani? Kitu gani utatamani ukikamilishe kabla hujafa? Yaandike majibu yote kutoka ndani yako sasa hayo ni mjibu ya wewe halisi.
Amua sasa kuachana nay eye feki kila unachokifanya jiulize hiki ni cha mimi orijino au yeye feki anataka kukushika tena? Weka maona yako kisha malengo na chochote utakachokuwa unakifanya kiwe kinatoka kwako wewe halisi. Hapo ndipo utakapoweza kupata chochote maishani mwako na kuwa na ridhiki moyoni mwako.
Imeandikwa na alfred mwanyika,
Mwanasayansi, mwl & mwandishi(uwezo wako halisi & mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz
