Yakimbilie Mambo Haya Matatu, Kila Kitu Kizuri Maishani Kitakukimbilia.
Rafiki yangu! Utajisikiaje kama leo utatambua mambo matatu ambayo ukiyakimbilia yatavuta mambo mengine yote mazuri kwenye maisha yako? Naamini utajisikia vizuri.
Habari njema ni kuwa makala hii itakuambia kwa wazi kabisa mambo hayo matatu.
Jambo la kwanza; Maarifa. Hata kitabu kitakatifu(Biblia) kinaweka wazi kuwa watu huangamizwa kwa kukosa maarifa.
Kumbe inawezekana umeangamia katika maeneo fulani ya maisha yako kwa kukosa maarifa. Maarifa hukuonyesha kipi kitu sahihi cha kufanya katika maisha yako.
Jambo la pili; Vitendo. Hata kama utakuwa unafahamu maarifa sahihi kiasi gani kama hutachukua hatua, basi ni bure tu. Hapa nazungumuzia kazi, ukishaweka malengo sahihi kinachofuata ni kuweka kazi.
Jambo la tatu; Ubora: Njia pekee ya kukufanya ukue ni leo kufanya vizuri kuliko jana.
Kufanya kwa ubora ndiyo kutakufanya upate matokeo bora. Kufanya kwa upekee ndiyo kutakupa matokeo ya pekee.
Ndugu haya ni mambo makubwa matatu uliyotakiwa kuyakimbilia kila siku ili kupata matokeo mazuri uliyoyatamani maishani mwako. Kama hujapata matokeo hayo basi tambua kuna mambo mengine uliyokuwa unayakimbilia huku ukiyaacha haya matatu.
Hapa unahitaji kubadili mwelekeo wa mambo yako. Mwelekeo huu ukusaidie kuanza kuyakimbilia mambo haya matatu kwenye kila eneo la maisha yako kama binafsi, fedha, mahusiano, kazi,biashara,….
Unaweza kuwa unajiuliza utaanzia wapi kuyakimbilia mambo haya matatu?
Usiwe na wasiwasi juu ya hilo. AMSHAUWEZO Consultant tumekuandalia semina iliyobebwa na kichwa PIGA U-TURN 101 ZA MAISHA YAKO. Kupitia semina hii utatambua mambo uliyokuwa unayakimbilia lakini hayakupatia matokeo unayoyataka maishani kisha kupiga U TURN(kugeuka) na kuyakimbilia mambo haya matatu kwa njia mbalimbali.
Mpaka mwisho wa semina utakuwa umetambua mambo 101 uliyokuwa unayakimbilia na yakakupa ugumu wa kupata matokeo kisha kuja na hatua 101 za kukimbilia maarifa, vitendo na ubora ili vingine vyote vikufuate.
Semina hii itafanyika kuanzia Julai 20 – 29, 2023 kwa njia ya kundi maalumu la wasap.
Ada ya semina hii ni sh 10,000/ unayolipia kupitia MPESA; 0752 206 899(Alfred Mwanyika). Pata picha unapata hatua sahihi 101 za kubadili uelekeo wa maisha yako, lazima upige hatua kubwa sana.
Ili kujihakikishia nafasi hii nakushauri ujiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hiki; https://chat.whatsapp.com/Lmel6ehEr30K5a1S1BCEYu
Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana na;
Mwl. Alfred Mwanyika
0752 206 899
www.amshauwezo.co.tz
Karibu sana.
