Ni Mpaka Ujinasue Kwenye Mitego Hii Mitano Ndipo Utaweza Kusonga Mbele .


Categories :

Je umekuwa ukiyatafuta mafanikio lakini kila  ukijitathmini unaona upo palepale? Je kila ukiyaona mafanikio makubwa kwa watu wengine unaona hao wamependelewa na wewe huwezi kuyapata?

Je ni kweli unataka kukata tamaa kwa sababu unaona umeshikwa sehemu na huwezi kujinasua? Ni mpaka ujinasue kwenye mitego hii mitano, ndipo utaweza kutoka hapo ulipo.

1. Mtego wa mtazamo hasi. Kwa kuamini wewe huwezi kufanya mambo makubwa , umekaribisha mambo madogo tu kisha kuyasukumia mbali mambo makubwa.

Unaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya hayo, lakini utaweza kama utabadili mtazamo na kuona una haki na uwezo wa kufanya makubwa.

2. Mtego wa Elimu ya shule. Unayafahamu mapito yako ya shule.  Ulipofeli na wakakuambia utafeli na maisha pia, umelibeba na unaliishi.
Uwezo mkubwa ulionao hauwezi kupimwa na mitihani ya darasani,  zinduka!

3. Mtego wa kushindwa kwako. Kwa nini bado umeshikilia kushindwa kwako? Hakuna kitu unachoweza kubadili kwenye kushindwa kulikopita kasoro kujifunza tu.

Usinaswe kwenye mtego wa kuendelea kujuta kwa yaliyopita. Jifunze kwayo kisha songa mbele. “Yaliyopita ni mfu kasoro uhai unayoyapa wewe”

4. Mafaniko yako ya sasa. Je ni elimu kubwa uliyonayo ndiyo inakupa kiburi cha kutofanya kitu chochote ila ajira? Je biashara yako kukua kwa haraka imekuchanganya kiasi cha kuanza kuwadharau wateja wako? Je mshahara unaoupata sasa unakufanya jidharau kazi?

Mafanikio yako yasikushike bali yawe ngazi ya kufikia mafanikio makubwa zaidi.

5. Mtego wa kuahirisha . Ni mara ngapi umeweka malengo na mipango mizuri ya kufanyia kazi lakini muda wa utekelezaji ukifika unasema nitafanya kesho? Kesho ikifika unasema kesho tena, miaka inaenda.

Ukipanga, weka kazi; hakuna MATOKEO bila KAZI.

Unaweza kutoka hapo uliponasa. Unaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya hayo uliyokwisha kufanya. Angalia ni mitego gani imekunasa kisha jinasue na kusonga mbele.

Hakikisha unakipata kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI. Huu ni mwongozo wa kukusaidia kujinasua hapo ulipo.  Utaanza kuweka kazi kisha kupata matokeo bila kupokea sababu yoyote ile.

Jipatie kitabu hiki leo kwa bei ya ofa.  Nakala chache za ofa zimebaki,  wahi ya kwako sasa. Wasiliana nasi 0752 206 899.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *