Kwani Wewe Umejaribu Mara Ngapi?Kwani Wewe Umejaribu Mara Ngapi?

Kila kitu ninachokifanya hakitiki! Kwani umejaribu mara ngapi? Mimi nyota yangu imefifia inabidi niende kwa mtaalamu aisafishe, mambo yangu hayaendi! Kwa umejaribu mara ngapi? Nilitaka kuwa mbobezi kwenye eneo hili lakini naona kama nipo palepale. Kwa wewe umefanya kwa muda gani? Nimefanya muda mrefu sana lakini sipati majibu, sasa naacha. [...]

Usipasue Yai Kuangalia Ukuuaji wa kifaranga, Subiri Muda Wake; Kitatoka tu!Usipasue Yai Kuangalia Ukuuaji wa kifaranga, Subiri Muda Wake; Kitatoka tu!

Unafahamu kuwa ili kifaranga cha kuku kiweze kupatikana basi ni lazima yai liatimiwe ama kwa kuku mwenye au kwa kutumia mashine. Kwa kulifahamu hilo umekuwa mwaminifu sana kusubiri kwa takribani siku 21 ili kukishuhudia kifaranga kikitoka. Hakuna hata siku moja uliposema natamani kuona kifaranga kinaendeleaje hivyo ukavunja yai ili kuona [...]

Tai Aliyegeuka Kuwa Kuku .Tai Aliyegeuka Kuwa Kuku .

“Toka Uliko, Una hadhi Ya daraja La Kwanza” Mwindaji mmoja akiwa porini alimuona tai akitoka kwenye kiota. Alipopanda kwenye mti uliokuwa na kiota hicho ndipo akalikuta yai moja, alilichukua na kwenda nalo nyumbani. Alipofika nyumbani akalichanganya lile yai na mayai ya kuku ambaye ndiyo alikuwa anaanza kuatamia. Baada ya siku [...]

Usisimamishe Nguzo Kabla Ya kuchimba Shimo….Itaanguka Tu!Usisimamishe Nguzo Kabla Ya kuchimba Shimo….Itaanguka Tu!

Kama utachukua nguzo na kuisimamisha juu ya ardhi bila kuichimbia shimo, tambua kabisa kuwa nguzo hiyo itaanguka tu. Hata kama utaamua kufanya kazi hiyo miaka elfu moja hutaweza kufanikiwa. Ili nguzo isimamishwe inahitaji kuchimbiwa shimo kisha nguzo hiyo kutumbukizwa na kushindiliwa. Umekuwa ukisimamisha nguzo maishani mwak, mpaka leo haijasimama na [...]

Usijifariji na Udogo Wa Jicho La Jipu…Ndani Yake Ni Kubwa SanaUsijifariji na Udogo Wa Jicho La Jipu…Ndani Yake Ni Kubwa Sana

Kama utatumia udogo wa jicho la jipu kuamu umakini kiasi gani uwekwe katika kushugulikia matibabu yake basi niseme utakuwa ‘umechemka’ sana. Mlango(jicho) wa jipu huonekana ni mdogo sana ukilinganisha na ukubwa wa jipu lenyewe ndani yake. Hivyo mtu angetumia tu kigezo cha ukubwa wa mlango huo angepuuzia sana matibabu yake [...]

Nguvu ya Maono Katika Kujenga Nidhamu Kali.
Nguvu ya Maono Katika Kujenga Nidhamu Kali.

“Dreva akishajikumbusha akilini mwake safari ndefu iliyopo mbele hujikuta akiongeza mwendokasi na kutamani sehemu nyingine magurudumu ya yasikanyage” Kama umeshawahi kupanda mabasi yanayokwenda masafa marefu kwa mfano Dar – Tunduma au Mwanza Dar utaelewa kauli hiyo hapo juu. Madreva wa mabasi kama hayo huwa na nidhamu kali sana. Nidhamu hiyo [...]

Toa Matokeo Sio SababuToa Matokeo Sio Sababu

Kuna kila sababu ya kwa nini usifanye kitu. Lakini kunahitaji kazi tu ili utoe matokeo. Sababu za kutokufanya kitu ni nyingi sana na hiki ndicho kilichopelekea watu wengi kukosa matokeo huku wakibakia na uthibitisho kwa nini hawana matokeo. Kutafuta sababu za kwa nini usifanye kile ulichopanga kufanya ni kutafuta raha [...]